17 Desemba 2019 - 09:07
Mahathir Mohammad: Vikwazo dhidi ya Iran ni aina fulani ya udikteta wa kimataifa

Mahathir Mohammad, Waziri Mkuu wa Malaysia sambamba na kupinga vikali vikazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amebainisha kwamba vikwazo hivyo ni aina fulani ya udikteta wa kimataifa.

(ABNA24.com) Dakta Mohammad ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Al Jazeera akiwa nchini Qatar ambapo ameenda huko kuhudhuria kongamano la mjini Doha.

Akishiaria vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na mahitajio ya soko la dunia, amesema kwamba, vikwazo hivyo havitaidhuru nchi moja pekee, bali nchi zote washirika wa Iran katika uga wa kiuchumi.

Waziri Mkuu wa Malaysia ameongeza kwamba, serikali ya nchi hiyo haiamini vikwazo wala mwenendo wa kuzishinikiza nchi nyingine zikubali idolojia fulani. Dakta Mahathir Mohammad amebainisha kwamba, wakati ulimwengu unazungumzia suala la  mataifa kuwa na mielekeo kadhaa ya kifikra, Marekani inaielekeza dunia upande usio sahihi.

Aidha Jumamosi iliyopita Waziri Mkuu wa Malaysia alivitaja vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni batili na vya kidhalimu. Aliendelea kubainisha kwamba nchi yake haitofuata vikwazo hivyo vya upande mmoja na ambavyo vinakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa na sheria zote za kimataifa.

Hivi karibuni Wizara ya Fedha ya Marekani na katika kuendeleza siasa zake za kimabavu na hatua zilizo kinyume cha sheria, iliiwekea Iran na washirika wake vikwazo vipya vya kibiashara, suala ambalo limekosolewa vikali kimataifa.

...........
340